KATIBA YA KLABU

KATIBA YA KLABU YA JIOGRAFIA NA HIFADHI YA MAZINGIRA

(GEOGRAPHY AND ENVIRONMENTAL CARE CLUB)

GECC

OF

ST ALFRED RULENGE SECONDARY SCHOOL.

 

UTANGULIZI 

“Klub hii ni hazina itakayochipuka na kukua”

Kwa waanzilishi wa Klabu hii, Mazingira na vitengo vyake ni kitu cha maana kabisa. Na hatuwezi kuacha kutafuta njia za kutekeleza namna ya kuyatunza na kuyahifadhi.  Kuanzia dakika hii wazo hili limeshaanza kuchipua na kukua.

Kwa muda wote wanachama na ikiwezekana watu wote, watajitoa kimuda, kifedha, kinguvu, na katika utayari wa kushirikiana  kwa ajili ya Mazingira.

Njia yetu inawezekana isiende jinsi tulivyofikiri bali tofauti. Wote watakaoshiriki huenda wakagundua kuwa watamhitaji kila mmoja kufanikisha pamoja jambo hili.

Basi,

Kwa kutambua umuhimu wa kuwa  na mazingira safi, yenye afya, yanayovutia na yaliyohifadhiwa kwa ajili ya  kuishi, kujifunzia na kufundishia hapa shuleni, kwa kuzingatia wajibu wetu, tunajiunga na kuanzisha Klabu ya jiografia na uhifadhi wa mazingira  kama katiba hii inavyoonesha.

 

Katiba hii ya Gecc itakuwa chini ya sheria mama ya shule.

 

 

 

 

 

  SURA  1

JINA, IMANI NA MADHUMUNI

Ibara ya 1  JINA

Klabu hii itajulikana kwa jina la Klabu ya jiografia na hifadhi ya mazingira  kwa kiingereza “GEOGRAPHY AND ENVIRONMENTAL CARE CLUB”  (GECC)

 Ibara ya 2  Imani:

i.                 Sisi wanaklabu tunaamini ukweli kwamba Kila kitu kilichoumbwa na Mungu  ni chema sana. (Mungu akaona kila kitu alichokifanya na tazama, ni chema sana” (mwanzo  1:31) Hivyo tunawiwa kutunza ulimwengu ili ubakie katika uzuri huo.

ii.               Ni dhahiri kwamba shughuli za binadamu zinaharibu uzuri wa uuumbaji huo, hivyo lazima zithibitiwe na zifanywe kwa tahadhari.

iii.              Sisi wanaklabu  tunatambua wajibu wetu wa kuhifadhi mazingira yetu na ya sayari dunia dhidi ya uharibifu na uchafuzi wote, kwani mazingira ni uhai.

iv.              Tunaamini tunu ya mazingira safi, yenye afya, yaliyohifadhiwa ni chachu ya ufanisi kitaaluma  na kwa mipango yote ya binadamu.

v.                Tunaamini katika uwezo wetu wa pamoja katika kuleta mabadiliko na kutunza mazingira yetu. Kwa pamoja tunaweza.

vi.              Tunaamini uharibifu wa mazingira unahatarisha maisha ya viumbe. Na kwamba ni juhudi zetu ndizo zitarekebisha hali hii. Hivyo lazima tujitolee na kujitoa kwa ajili ya kazi ya pekee ya kuhakikisha  mazingira safi na bora.

 

 

 

Ibara  ya 3  MADHUMUNI

Kusaidia shule katika kuboresha mazingira kwa kuhakikisha usafi na uhifadhi hasa:

i.                 Kusaidia shule katika kutoa elimu bora na endelevu ya mazingira, kukuza maarifa na ujuzi wa mazingira  kwa namna mbali mbali, kwa maneno na matendo.

ii.               Kufanya utetezi na ushawishi wa masuala ya mazingira na sera zilizopo.

iii.              Kulea tabia njema ya usafi na uhifadhi wa mazingira ili wanafunzi wawe na mtazamo wa kuwa wana mazingira sasa na  baadae.

iv.              Kufanya tafiti shirikishi, kusoma tafiti na kutoa ripoti za kitaalamu kuhusu mazingira ya shule na katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

v.                Kuwajengea  wanajumuiya uwezo wa kumudu shughuli za uhifadhi wa mazingira kwa njia ya semina, makongamano, hotuba, mafunzo na shughuli za uhifadhi.

vi.              Kuwa chachu na chombo thabiti cha kuhifadhi mazingira kwa kuongoza wengine katika kuyalinda mazingira.

vii.            Kuhamasisha utalii wa ndani na nje kwa maendeleo ya nchi.

viii.           Kuhakikisha mazingira safi, yanayovutia, yenye afya  na yaliyohifadhiwa ili kuchangia ufanisi kitaaluma.

ix.              Kuibua miradi na kutumia fursa zilizopo ili kuondoa kero za kimazingira.

x.                Kutoa ushauri kuhusu masuala yanayohitaji kushugulikiwa kufikia mazingira safi na vitengo vyake.

xi.              Kufanya utandawishaji wa shughuli za uhifadhi ndani na nje ya shule, kitaifa na kimataifa.

xii.            Kudhibiti uwezekano wa uharibifu wa mazingira wa namna yoyote ile.

xiii.           GECC itashirikiana na wadau wengine kwingineko ili kuhakikisha malengo yote yanatimia.(partnership)

xiv.           Wanaklabu watashirikiana na kushirikishwa ili kuendeleza GECC.

                                    

 SURA YA 2

UANACHAMA

Ibara 4  Uanachama utakuwa kwa:

i.                 Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Mt Alfred  Rulenge ikiwa 

a.     Atakubaliana na katiba Ya GECC.

b.     Atalipa kiingilio na ada na kupewa kadi ya uanachama.

c.      Atalipa ada ya mwaka na michango iliyopangwa.

d.     Ataudhuria vikao, mikutano na shughuli zingine zitakazopangwa na wanaklabu wenyewe kwa uamninifu.

e.     Anapenda mazingira, pamoja naviumbe  na anakerwa na uharibifu wa aina yoyote.

Ibara 5 kupoteza uanachama

i.                 Mwanaklabu atapoteza uanachama wake endapo atashindwa kutimiza au kukiuka ibara ya 4 ya katiba hii.

ii.               Mwana klabu atapoteza uanachama wake endapo atakosa nia thabiti ya kupenda na kuhifadhi mazingira.

iii.              Atafukuzwa kwa mujibu wa sheria.

Ibara ya 6   cheti

i.                 Mwanachama atapokea cheti wakati wa kuhitimu masomo kulingana na kiwango chake cha Elimu yake.

ii.               Cheti cha GECC kitatolewa na Klabu na kuthibitishwa na mkuu wa shule pamoja na mlezi wa klabu.

 

                                                 SURA 3

                                        MUUNDO WA KLABU:

Ibara 7   Kamati kuu ya utendaji ya Klabu

i.                 Watakaohudhuria watakuwa-

a.     Mwenyekiti

b.     Makamu mwenyekiti

c.      Katibu

d.     Katibu msaidizi

e.     Mtunza hazina

f.       Mwalimu mshauri

g.      Mwalimu mlezi

ii.               Wajibu wa kamati kuu tendaji utakuwa

a.     Kuandaa agenda za kikao cha halmashauri kuu ya klabu

b.     Kutekeleza maazimio ya Halmashauri kuu ya Klabu.

c.      Kuandaa taarifa itakayotolewa kwenye kikao cha mkutano mkuu wa klabu

d.     Kufanya vikao visivyopungua vitatu kwa muhula.

e.     Kuandaa taarifa itakayotolewa kwenye kikao cha bodi ya ushauri.

 

Ibara 8 Halmashauri kuu ya klabu

i.                 Watakaoudhuria watakuwa:-

a.     Kamati kuu tendaji ya Klabu

b.     Wajumbe wawili waliochaguliwa na mkutano mkuu wa klabu.

c.      Viongozi wa kamati mbalimbali (mwenyekiti na katibu wa kamati)

d.     Wataalamu wa kualikwa (hawa ni washiriki washauri hawana haki kupiga kura)

 

ii.               Wajibu wa halmashauri kuu utakuwa

a.     Kuangalia shughuli zote za maendeleo ya GECC

b.     Kusimamia utekelezaji wa maazimio ya mkutano mkuu.

c.      Kuunda kamati mbalimbali kama itakavyoona inafaa kwa mujibu wa katiba hii.

d.     Kupokea kujadili,kujadili na kupitisha taarifa ya utendaji wa kamati kuu tendaji itakayotolewa kwenye mkutano mkuu wa klabu.

e.     Kupokea taarifa za kamati mbalimbali na kuzijadili.

f.       Kupokea taarifa ya bodi ya ushauri na kutoa maamuzi.

g.      Kuandaa agenda za mkutano mkuu wa klabu.

h.     Kufanya vikao visivyopungua vitatu kwa mwaka.

Ibara 9  Mkutano mkuu wa Klabu.

(i)               Watakaoudhuria watakuwa:-

a.     Kamati kuu ya Klabu.

b.     Wanaklabu wote.

c.      Mwalimu mshauri wa Klabu.

d.     Mwalimu mlezi

e.     Mkuu wa shule.

f.       Mjumbe wa serikali ya wanafunzi.

(ii)             Wajibu wa mkutano mkuu utakuwa:-

a.     Kuchagua viongozi wa Klabu (mwenyekiti, makamu, katibu, makamu, mtunza hazina, msaidizi, wajumbe wawili wa bodi ya ushauri wa klabu na wajumbe wawili wa halmashauri ya Klabu.

b.     Kupokea na kujadili taarifa ya halmashauri kuu ya klabu na kutoa maamuzi.

c.      Kupokea na kujadili taarifa ya bodi ya ushauri ya klabu.

d.     Kufanya mkutano mkuu mara mbili kwa mwaka wa kwanza ukiwa ni tathmini baada ya miezi sita na wa pili utahusisha uchaguzi.

 

FUNGU LA PILI

Ibara ya 10; Bodi ya washauri ya klabu:

(i)               Kutakuwepo na bodi ya washauri watakao udhuria watakuwa:-

a.     Mkuu wa shule.

b.     Mwalimu wa mazingira na usafi/kazi

c.      Mwalimu mshauri

d.     Mwalimu mlezi.

e.     Rais wa klabu.

f.       Wajumbe wawili waliochaguliwa na mkutano mkuu.

(ii)             Wajibu wa bodi ya ushauri utakuwa:-

a.     Kupokea na kujadili taarifa ya mkutano mkuu wa klabu na kutoa ushauri.

b.     Kuidhinisha bajeti ya klabu kwa mwaka wa fedha unaofuata.

c.      Kufanya  mkutano mara mbili kwa mwaka  ikufuatia mkutano mkuu.

                                                           SURA YA 4

                                                                UONGOZI

Ibara ya 11   viongozi

i)                 Katika klabu hii kutakuwa na viongozi wafuatao:

a.     Mwenyekiti / rais

b.     Makamu mwenyekiti

c.      Katibu

d.     Katibu msaidizi

e.     Mtunza hazina

 

ii)               Wajibu wa rais /mwenyekiti

a.     Kuongoza mikutano na vikao vyote vya kamati kuu, halmashauri kuu na mkutano mkuu.

b.     Ni katibu wa bodi ya ushauri.

c.      Kutunza taratibu katika mikutano na vikao

d.     Kupiga kura ya uamuzi kwenye vikao na mikutano ikiwa kura zinalingana.

e.     Kuitisha kikao cha kamati kuu kwa njia ya katibu, ili mradi yeye mwenyewe au makamu atahudhuria kikao hicho

f.       Kusoma taarifa ya utendaji wa mwaka mbele ya mkutano mkuu na halmashauri kuu kwa niaba ya kamati kuu.

g.      Kubeba dhamana ya mali zote za Klabu katika ngazi husika.

h.     Makamu wa rais/makamu mwenyekiti au kazi zote za rais /mwenyekiti kama hatakuwepo au atajiuzulu.

 

iii)             Wajibu wa katibu mkuu

a.     Ndiye mtendaji wa shughuli zote katika klabu

b.     Atashughulikia barua zote, atatunza daftari (register book) la klabu na miniti zote za Klabu.

c.      Ni mwandishi wa vikao vyote vya kamati kuu, hlamashauri kuu na mkutano mkuu.

d.     Kubeba dhamana ya mali zote za klabu.

e.     Katibu msaidizi atafanya kazi zote atakapoagizwa na katibu au kazi zote za katibu kama hatakuwepo au atajiuzulu.

 

 

iv)              Wajibu wa mtunza hazina:

a.     Kupokea na kutoa fedha kwa shughuli zote za klabu.

b.     Kutoa stakabadhi kwa kila fedha takayopokea.

c.      Kuhakikisha fedha zimewekwa katika akaunti ya klabu ofisi ya msalifu.

d.     Kutunza vitabu vyote vya fedha.

e.     Kutoa taarifa ya fedha ya mwaka mbele ya halmashauri kuu na mkutano mkuu.

f.       Kubeba dhamana na mali zote za Klabu.

g.      Mtunza hazina ni mmoja wa watia saini kuidhinisha kutoa/kuweka fedha kwa mhasibu/benki.

 

v)               Ibara ya 12   MIIKO YA UONGOZI

(i)               Viongozi wote watatokana na wanachama wa klabu tu.

(ii)             Viongozi wote wa klabu watatii na kutekeleza katiba hii.

(iii)           Viongozi wote wawe mfano katika kupenda na kuhifadhi mazingira.

(iv)            Viongozi watathibitishwa na mwalimu mlezi/mshauri.

(v)             Kiongozi atapoteza nafasi yake ya uongozi ikiwa atakuwa amepoteza uanachama wake kwa mujibu wa ibara ya tano.

(vi)            Kiongozi akipoteza sifa za uongozi atasimamishwa mara moja na kamati kuu na suala lake kujadiliwa katika kikao cha halmashauri kuu ya klabu.

(vii)          Nafasi itakayoachwa wazi kutokana na kiongozi kupoteza sifa/kujiuzulu/kufariki/kuhama na ugonjwa wa muda mrefu, nafasi yake itajazwa na halmashauri kuu pekee.

(viii)        Kiongozi awe mfano asipokee wala kutoa rushwa.

(ix)            Kiongozi asitumie madaraka yakee vibaya ili kujinufaisha mwenyewe.

                                                    

                                                             SURA YA 5 

                                                            UCHAGUZI

Ibara ya 13   Muda wa uchaguzi;

(i)               Uchaguzi utafanyika kila baada ya mwaka mmoja.

(ii)             Uchaguzi uzingatie utaratibu wa mihula ya shule.

(iii)           Uchaguzi wa viongozi ufanyike kila mwaka kati ya julai na September inafaa baada ya uchaguzi wa serikali ya wanafunzi.

Ibara ya 14  Msimamizi wa uchaguzi 

(i)               Uchaguzi utasimamiwa na mlezi wa klabu.

(ii)             Pia kutakuwepo na kamati ya uchaguzi ya klabu.

Ibara 15  kupiga kura:

(i)               Uchaguzi utakuwa wa siri.

(ii)             Majina matatu yatayoungwa mkono na zaidi ya nusu ya wapiga kura yataingia katika uchaguzi.

(iii)           Kama hakuna atakayepata zaidi ya nusu ya wapiga kura, uchaguzi urudiwe kati ya wale wawili waliopata kura nyingi.

(iv)            Kama kuna kufungana kwa kura, msimamizi wa uchaguzi atakuwa na kura ya uamuzi.

(v)             Mlezi/mshauri hatapiga kura.

 

Ibara ya 16  Baada ya uchaguzi:

                            i.          Viongozi wapya watatangazwa na msimamizi wa uchaguzi kwenye mkutano husika.

                           ii.          Makabidhiano ya kumbukumbu za klabu yafanyike siku hiyo.

 

SURA YA 6

VIKAO  NA MIKUTANO:

Ibara ya 17

Vikao vya kamati kuu na Halmashauri kuu vitafanyika ikiwa wajumbe wasiopungua nusu wataudhuria.

Ibara ya 18 mikutano:

Mkutano mkuu wa klabu utafanyika ikiwa wajumbe wasiopungua nusu wataudhuria.

 

 

SURA YA 8

WALEZI NA WASHAURI

Ibara ya 19  mwalimu mwanzilishi klabu

i. Ndiye mlezi mkuu wa klabu.

ii. Anaweza kuteuliwa mwalimu mshauri miongoni mwa walimu kuwa mshauri wa klabu kwa maombi ya mkutano mkuu wa klabu.

iii. Mkuu wa shule pia anaweza kuwa mlezi mkuu wa Klabu na akateuliwa mwalimu mshauri.

A. watashirikiana katika kulea klabu.

      B.  Wakuwa viungo kati ya uongozi wa shule na wanaklabu.

      C.Wataudhuria mikutano yote itakayoitishwa na mwenyekiti.

D.Mlezi anaweza kukaa kwa kipindi cha miaka 2 na anaweza kuombwa tena kuendelea(kama si muasisi)

 

SURA YA 9

    FEDHA NA MIRADI YA KLABU

Ibara ya 20  ada na michango

          i.          Kila mwanachama mpya atalipa kiingilio.

        ii.          Kila mwanaklabu atalipa ada ya uanachama kila mwaka.

       iii.          Kima cha mchango kitapangwa na halmashauri kuu ya klabu.

       iv.          Mwalimu mlezi/mshauri atalipa ada kama itakavyopangwa na halmashauri kuu.

Ibara ya 21  utunzaji na ukaguzi wa mahesabu ya fedha.

                            i.          Fedha zote zihifadhiwe kwa mhasibu wa shule/mkuu wa shule.

                           ii.          Akaunti ya Klabu itatunzwa na kamati kuu ya klabu.

                         iii.          Mfuko wa klabu utatumika kwa madhumuni ya kuendeleza shughuli za klabu ilimradi matumizi yake hayatazidi mapato.

                         iv.          Hesabu za klabu zitakaguliwa kila mwaka kabla ya mkutano mkuu na mtu atakayechaguliwa na halmashauri kuu.

                           v.          Watia saini katika akaunti watakuwa mwenyekiti, mtunza hazina mwalimu mshauri/mlezi.

 

Ibara 22  Sera ya fedha:

                                      i.          Kutakuwa na sera ya fedha itakayothibitishwa na kikao cha halmashauri kuu ya klabu.

                                     ii.          Kamati kuu ya klabu itasimamia utekelezaji wa sera ya fedha.

Ibara ya 23: Miradi

Klabu itabuni na kuendesha miradi mbalimbali ya uzalishaji kwa ajili ya maendeleo ya klabu. Miradi yote itakayoanzishwa iwe imeidhinishwa na halmashauri kuu  na iwe ile inayozingatia hali halisi ya hapa shuleni.

Ibara 24 Umiliki wa mali:

       i.          Klabu itamiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika.

     ii.          Kamati kuu ndiyo yenye dhamana ya kutunza mali zote za klabu kwa kutumia daftari la kumbukumbu  (register book)

SURA YA 10

MAREKEBISHO YA KATIBA

Ibara ya 25  Muda wa marekebisho ya katiba

       i.          Katiba itaangaliwa upya kila baada ya miaka mitano ila marekebisho madogo yanaweza kufanyika kabla ya muda huo kwa mujibu wa katiba hii ibara ya 25.

     ii.          Mwanaklabu anaweza kupendekeza marekebisho ya katiba kwa kufuata utaratibu huu ufuatao:

a.     Pendekezo linaungwa mkono na nusu ya wajumbe rasmi waliopo katika mkutano mkuu wa mwaka.

b.     Mapendekezo yote yajadiliwe na halmashauri kuu.

c.      Rekebisho lolote la katiba litapitishwa endapo theluthi mbili 2/3 ya wajumbe wa mkutano mkuu wa klabu wataliunga mkono.

d.     Rekebisho lolote lazima liungwe mkono na mlezi.

Ibara ya 26:  Kamati ya katiba

a.     kutakuwa na kamati ya katiba ambayo wajumbe wake ni rais, katibu kuu na wajumbe watano wa kuchaguliwa na mkutano mkuu.

b.     Kamati ya katiba itaundwa muda wowote na itadumu kwa miaka mitatu.

 

Nyongeza

(a)   Klabu itafanya kumbukumbu za kuasisiwa kila mwaka mwezi September kati ya tarehe 20 na 25.

(b)   Klabu itakuwa na utambulisho maalum yaani Nembo ya Klabu, wimbo wa klabu na Sala ya Klabu itakayofaamika na wanaklabu wote.

(c)    Ni shariti kila atakayepewa wajibu katika klabu hii kusaidia klabu ili ipige hatua moja au zaidi kwa uhakika ili shughuli zake ziwe hai na endelevu.

 

                      MUNGU IBARIKI KLABU YETU, MUNGU IBARIKI SHULE YETU.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


Comments

Popular posts from this blog

WELCOME TO OUR CLUB

KEEP TANZANIA CLEAN